Business

header ads

RAIS MAGUFULI ATOA NAFASI KWA WABUNGE WAWILI

Elikunda Materu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, leo Septemba 9, 2018 amefanya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali ambapo katika uteuzi huo amewajumuisha wabunge wawili wa zamani.


Magufuli amemteua Ndg. Stephen Masato Wasira kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Ndg. Wasira anachukua nafasi ya Prof. Mark James Mwandosya.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Festus Bulugu Limbu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (National Economic Empowerment Council – NEEC).
Dkt. Limbu anachukua nafasi ya Dkt. John Jingu ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto).
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 09 Septemba, 2018.

Post a Comment

0 Comments