Business

header ads

MTUHUMIWA UJAMBAZI SUGU AKAMATWA SONGWE

Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, linamshikilia mtu mmoja ambaye amekuwa akijihusisha na matukio mbalimbali ikiwemo, ujambazi, utapeli kwa kutumia nembo za freemason, akiwa na silaha aina ya  Air Gun  pamoja na risasi 135.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mathias Nyange amesema, mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Jerico Chifunda Msukuma, ni mkazi Nazareti Mjini Tunduma.
Mbali na kukutwa na vitu hivyo pia amekutwa na vitambulisho vinavyoonesha uraia wa nchi mbili Tanzania na Zambia ambapo anadaiwa kufanya matukio ya uhalifu kisha kukimbilia nchini Zambia.
Vitu vingine ambavyo amekutwa navyo Msukuma ni pamoja na jeneza dogo, pingu,  pasi inayotumika kutapeli watu kupata fedha, mashine ya kunakilisha  noti bandia, na karatasi zinazolingana ukubwa na noti ya shilingi 10,000.
Katika Hatua nyingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu 12 wakiwa na   vitu mbalimbali vya kama luninga, na radio, ambavyo vimeibwa katika matukio mbalimbali  na kwamba tayari vimetambuliwa na wamiliki.
Aidha, Kamanda Nyange ametoa Wito kwa Jamii kutowaamini watu wanaotumia imani za kishirikina kudai kwa watapata utajiri  na mafanikio ya haraka badala yake wafanye kazi kwa njia halali. Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapo kamilika.

Post a Comment

0 Comments