Business

header ads

UKITAKA LAIN YA PILI KUANDIKA BARUA TCRANa Oliver Nyeriga 
Serikali imesema kuwa imeanza kuchukua hatua za kudhibiti umiliki holela wa laini za simu nchini ambapo chini ya utaratibu mpya unaoandaliwa wa usajili wa simu kwa kutumia alama ya vidole mtu atakayetaka kusajili laini ya simu zaidi ya moja sasa atapaswa kuandika barua ya maombi ya laini hiyo ya pili.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditie ameyasema hayo leo katika mahojiano maaluma na EATV SAA 1 ilipotaka kujua njia zipi mpya ambazo serikali imekujanazo katika kuhakikisha wanadhibiti uhalifu kwa njia ya mtandao.

Mhandisi Nditiye amesema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA wameanza usajili kwa kuchukua alama muhimu za mwili kama sura na alama za vidole na kwa wale watakaohitaji line zaidi ya moja watatakiwa kuandika barua ya maelezo kisheria kwanini wapewe line zaidi ya moja.

Katika hatua nyingine Mhandisi Nditie amesema wanahakikisha usalama wa mawasiliano nchini hauingiliani na nchi jirani hivyo wamefanya mazungumzo na nchi zilizopo pembezoni mwa Tanzania ili zichukue hatua za kudhibiti muingiliano wa masafa ya simu ya nchi zao hasa maeneo ya mipakani ambayo ndio kumekuwa na changamoto kubwa ya muingilino huo na kuleta usumbufu kwa watumiaji wa mitandao hiyo nchini.

Post a Comment

0 Comments