Business

header ads

MWANAMUZIKI ARETHA FRANKLIN AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki Mkongwe wa muziki wa 'Soul Music' kutoka nchini Marekani Aretha franklin amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na Kansa ya Kongosho "Pancreatic Cancer" kwa muda mrefu.

Mara ya mwisho kuonekana stejini akiperform ilikua June mwaka 2017 mjini Detroit na baada ya kumaliza show hiyo aliwaomba watu wamuombee. "God Bless You, God Keep You, Keep Me In Your Prayers". Akiwa na umri wa miaka 14 alikua tayari ameachia album yake aliyoipa jina "Songs of Faith" 
Anetha Franklin alitamba na hit songs kama "Respect" , "Chain of Fools" , "Call me" na nyimbo zingine kali.

Anetha Franklin alishinda Grammy awards mara 18 mwaka 1968 na ameshafanya kazi na waimbaji maarufu kama Mary J Blidge kwenye wimbo wa Gospel ulioshinda Best Gospel-Soul Vocal Perfomance by a Duo or Group "Never Gonna Break My Faith" mwaka 2008.

Post a Comment

0 Comments