Business

header ads

MFUMUKO WA BEI MWEZI JULY WAPUNGUAOfisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa mfumuko wa bei kwa mwezi Julai mwaka huu umepungua hadi kufikia asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 3.4 ilivyokuwa mwezi Juni.

Kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei ya baadhi ya bidhaa za vya kula.

Kila mwezi NBS hutoa taarifa za takwimu kwa ajili ya kuwawezesha watunga sera kutekeleza majukumu yao kwa ajili ya manufaa ya taifa na ofisi hiyo imeeleza mfumuko wa bei kwa taifa kwa mwezi julai mwaka huu umepungua hadi kufikia asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 3.4 kwa mwezi juni mwaka huu.

Katika kipindi cha miaka kumi na saba iliyopita mfumuko wa bei haujawahi kushuka kwa kiasi hicho cha asilimia 3.3.

Wafanyabiasha wa soko la majengo jijini Dodoma wamesema kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei katika kipindi hiki kumetokana na kuongezeka kwa bidhaa nyingi hali iliyosababishwa na kunyesha kwa mvua nyingi na kupelekea mavuno mengi.


Katika baadhi ya nchi za afrika mashariki hali ya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioisha Julai 2018, Uganda imeongezeka kwa asilimia 3.1 kutoka asilimia 2.2 Kenya umeongezeka kwa asilimia 4.35 kutoka asilimia 4.28.


Post a Comment

0 Comments