Business

header ads

MBUNGE HAONGA NA WENZAKE WAACHIWA HURUMahakama ya Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe imemuachia huru mbunge wa Mbozi kupitia chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Pascal Haonga na wenzake wawili baada ya kukutwa hawana hatia katika kesi iliyokuwa ikiwakabili.


Katika kesi hiyo Haonga, Katibu wake Wilfredy Mwalusamba na Mashaka Mwampashi Walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ya kufanya fujo na kuvuruga mkutano wa uchaguzi wa baraza la mji mdogo wa Mlowo, kosa la pili na tatu ni kuwazuia askari kutekeleza majukumu yao makosa waliyodaiwa kuyatenda Agost 28 mwaka 2017.

Akisoma huku hiyo leo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Nemes Chami amesema katika mashtaka yote matatu, upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha makosa.

Amesema kuwa katika ushihidi wa mashahidi sita wa upande wa Jamhuri hakuna mahali walipothibitisha kwamba washtakiwa walikataa kukamatwa na kuwa hakuna mahali walipoonesha kwamba washtakiwa hawa waliwazuia askari kutekeleza majukumu yao na hakuna mahali walipothibitisha kwamba washtakiwa walilazimisha kurudi ukumbini baada ya kutolewa nje.

Amesema kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha ushahidi wa mashtaka waliyoyawasilisha mahakamani hapo, mahakama inawaachiria huru washtakiwa wote pamoja na kueleza kama kuna upande unaona haujaridhika na hukumu hiyo una haki ya kukataa rufaa ndani ya muda wa kisheria.

Post a Comment

0 Comments