Business

header ads

JESHI LA POLISI KUCHUNGUZA TUKIO LA KUPIGWA KWA MWANDISHI
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema polisi imeanza uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa mwandishi wa habari wa Wapo Redio, Sillas Mbise.

Akizungumza leo Ijumaa Agosti 10, 2018 Mambosasa amesema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha hizo za video ambapo Mbise anadaiwa kushambuliwa na polisi juzi Agosti 8, 2018 wakati wa mchezo kati ya Simba na Asante Kotoko ya Ghana.

Amesema hiyo inakwenda sambamba na kumtaka mtendewa wa kosa hilo la kupigwa kutoa taarifa kituo cha polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

“mtu yeyote anatakiwa kutoa malalamiko yake pale anapoona ametendewa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria”amesema Mambosasa

Wakati huo huo watetezi wa haki za binadamu wametoa matamko yao wakiwemo Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) .

Kupitia mwakilishi wake Edwin Soko amesema kuwa chama hicho kinalaani vikali tukio la kupigwa kwa Mwandishi wa habari za Michezo wa WAPO Redio aitwaye Sillas Mbise lililofanywa na Jeshi la Polisi Agosti 8, 2018, kwenye mchezo wa kuchagiza Simba Day kati ya Timu ya Simba mabingwa wa VPL na Ahsante Kotoko toka Nchi ya Ghana

Amesema OJADACT inapiga vita uhalifu, na shambulio la Mbise ni uhalifu wa kudhuru mwili, hivyo tumesikitishwa sana na tukio hilo, kwani linamdhalilisha Mwandishi huyo, kuidhalilisha tasnia ya habari na kuwavunja moyo waandishi wa michezo.

Pia wametoa rai kwa Rais wa TFF, kuwa na mikakati mathubuti ya kuandaa mazingira salama kwa waandishi wa habari za michezo, wanapoingia viwanjani, wanapotekeleza majukumu yao na kutoka viwanjani, ili kulinda heshima ya soka la Tanzania.

Post a Comment

0 Comments