Business

header ads

HAWA HAPA WABUNGE WATEULE CHADEMA, KOROGWE,UKONGA, MONDULI

 MGOMBEA JIMBO LA UKONGA ASIA MSANGI 
MGOMBEA JIMBO LA KOROGWE AMINA SAGUTI 

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imeteua wagombea wake wa ubunge katika majimbo matatu.

Walioteuliwa na majimbo watakayowania katika mabano ni Asia Msangi (Ukonga), Amina Saguti (Korogwe Vijijini) na Yonas Laiser (Monduli).

Taarifa ya Chadema iliyotolewa leo na mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene imesema wagombea hao wamepitishwa katika kikao maalum cha kamati kuu kilichoketi kwa siku mbili kati ya juzi na jana.

Amesema Kamati Kuu ya Chama imefanya uteuzi huo wa wagombea ubunge kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 2006, toleo la mwaka 2016, ibara ya 7.7.16(q).

Wagombea hao wanatarajiwa kuchuana vikali na wagombea waliopitishwa na kamati kuu ya CCM siku chache zilizopia ambao ni Julius Kalanga Laizer jimbo la Monduli, Mwita Mikwabe Waitara jimbo la Ukonga na Timotheo Paul Mzava jimbo la Korogwe Vijijini.

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kufanyika Septemba 16, mwaka huu baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza Uchaguzi majimbo hayo kuwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa Ukonga Mwita Waitara kuhamia CCM kutoka Chadema, hivyo katika jimbo la Monduli Julius Kalanga kuhamia CCM kutoka Chadema na jimbo la Korogwe baada ya kufariki kwa Mbunge wake Stephen Ngonyani.

Post a Comment

0 Comments