Business

header ads

FACEBOOK KUSITISHA UWEKEZAJI UGANDA

Mtandao wa Kijamii wa Facebook, umeonya kwamba, utasitisha mpango wake wa kuwekeza kwenye miundombinu yenye thamani ya mamilioni ya Dola nchini Uganda kufuatia hatua ya serikali ya nchi hiyo kutoza kodi watumiaji wa mitandao nchini humo.
Meneja wa Sera za Umma kwa Afrika wa Facebook, Kojo Boakye, amesema, wameiarifu Tume ya Mawasiliano Uganda, kwamba uwekezaji huo utahamishiwa nchi nyingine na kuongeza kuwa mfumo wa uwekezaji walioupanga nchini Uganda utaathiriwa kwa kodi hiyo.Mtandao huo ulitangazwa uwekezaji wake wa kwanza nchini Uganda mwaka 2017 ambapo ulipanga kushirikiana na Airtel Uganda, Bandwidth na kampuni ya Cloud Services kuuongeza mkongo wa mawasiliano wenye urefu wa kilomita 770 kuelekea kaskazini nchi hiyo.
Hata hivyo, Waziri wa Mipango wa Uganda, David Bahati, amedai, kwamba moja ya sababu za kuanzishwa kwa kodi ya wattumiaji wa mitandao ni kukusanya fedha kwa ajili ya kutanua huduma za intaneti hadi maeneo ya vijijini nchini humo.Kwa mujibu wa Bw. Bahati serikali inahitaji zaidi ya Dola milioni 536.3 kupanua wigo wa huduma za intaneti vijijini.

Post a Comment

0 Comments