Business

header ads

WEMA SEPETU JELA MWAKA MMOJA AU FAINI MIL 2


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, kulipa faini ya Shilingi milioni moja kwa kila kosa au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kutumia na kukutwa na dawa za kulevya aina bangi.

Hukumu hiyo imetolewa leo, na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kumtia hatiani kama alivyoshtakiwa.

Pia mahakama hiyo imewaachia huru mshtakiwa wa pili na watatu, katika kesi hiyo, ambao ni wafanyakazi wa Wema, Angelina Msigwa na Matirda Abas.

Wema Sepetu ni moja ya wasanii ambao waliwahi kutajwa katika orodha ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ya watu wanaohusika na kutumia au kuuza dawa za kulevya Februari 06, 2017.

TAZAMA https://youtu.be/OaRr7Rbbv7s


Post a Comment

0 Comments