Business

header ads

RAIS WA USWISI AFANYA ZIARA BINAFSI YA SIKU 14 TANZANIA


Rais wa Uswisi Mhe. Alain Berset ameahidi kuhamasisha wananchi nchini kwake kuja Tanzania kutalii na kuwekeza katika sekta ya utalii ambayo ameisifia kutokana na uzuri wa vivutio vyake vingi pamoja na amani na utulivu uliopo nchini.


Rais Berset amesema hayo wakati akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Jumatano usiku.

Rais huyo wa Uswisi alikuwa akijiandaa kuondoka kurudi nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake binafsi ambapo alitembelea hifadhi za Taifa na Zanzibar kwa muda wa siku 14 akiwa pamoja na familia yake.

Kwa upande wake Waziri Mahiga amesema ujio wa Rais huyo wa Uswisi pamoja na familia yake ni mwendelezo wa kuja kwa watu mashuhuri nchini ikiwa ni pamoja na viongozi wa dunia wanaopendelea kuzuru vivutio mbalimbali vya kitalii nchini kwa faragha.

Amesema hivi sasa kuna ongezeko kubwa sana la watalii viongozi na watu mashuhuri mbalimbali kwa kuwa Tanzania imekuwa ikiheshimu matakwa yao ya ufaragha, jambo ambalo amesema limekuwa chachu na kivutio kikuu cha ongezeko la watu wa aina hiyo.


Post a Comment

0 Comments