Business

header ads

MATOKEO KIDATO CHA SITA SHULE YA WASICHANA JANGWANI KATIKA ORODHA YA WASHIKA MKIABaraza la mtihani la taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita leo na kubainisha kufuta matokeo ya watahiniwa wanane, waliofanya mtihani wa kidato cha sita kutokana na udanganyifu.

Akitangaza matokeo hayo leo mjini Zanzibar Katibu Mtendaji wa Necta, Charles Msonde amesema watahaniwa hao walibainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani ambapo kati ya watahiniwa hao wanane waliofutiwa matokeo, wanne ni wa shule na wanne ni wa kujitegemea.

Akieleza kiwango cha ufaulu Dkt. Msonde amesema kuwa ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 96.06% mwaka 2017 hadi 97.12% mwaka huu, huku ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka ukilinganishwa na masomo ya sanaa na biashara.

Amesema jumla ya watahiniwa 83,581 sawa na asilimia 97.58 ya watahiniwa waliofanya mitihani ya kidato cha sita Mei mwaka huu wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 34,358, na wavulana waliofaulu ni 49,223 pekee.

Dkt. Msonde ameongeza kuwa tathmini ya hali ya matokeo imeonesha kuimarika kwa ufaulu katika madaraja ya I,II na III ikiwemo kupanda kwa asilimia 1.80 kutoka 93.72 mwaka 2017 na kuwa asilimia 95.52 mwaka 2018.

Amezitaja shule zilizoongoza katika matokeo hayo ni pamoja na Kibaha, Kisimiri, kemebos na Mzumbe, Shule nyingine zilizoshika kumi bora, ni Feza Boy’s, Marian Boys ,Ahmes, St Mar’ys Mazinde Juu, Marian Girls na Feza Girls’s.

Pia amezitaja Shule nyingine zilizoshika mkia ni shule ya wasichana ya Jangwani, ya Jijini Dar es Salaam. Forest ya (Morogoro), Jang’ombe, St James, Kilolo,(Iringa), White Lake,(Dar es Salaam) Aggrey,(Mbeya), Nyailigamba,(Kagera) Musoma Utalii, (Mara) Ben Bella(Mjini Magharibi) na Golde Ridge(Geita).Post a Comment

0 Comments