Business

header ads

MAKADA SITA UPINZANI WAREJEA CCM

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) kimemrejeshea uanachama mwanachama wake aliyefukuzwa kwenye chama Bi. Sophia Simba baada ya kuandika barua mara kwa mara  za kuomba msamaha.
Wajumbe wa kikao hicho kilichofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. John Magufuli, kwa pamoja wameridhia kumsamehe mwanasiasa huyo mkongwe ambaye aliwahi kukitumikia chama hicho katika nafasi mbalimbali.
Kikao hicho pia kimetoa ridhaa ya kurejea tena CCM kwa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha aliyeachana na Chadema pamoja na kumpokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema- Taifa Patrobas Katambi, wanachama wa ACT- Wazalendo Albert  Msando, Samson Mwigamba na Edna Sunga.

Post a Comment

0 Comments