Business

header ads

SERIKALI KUFUTA KODI YA TAULO ZA KIKE "PEDI"
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto mh. Ummy Mwalimu amesema majadiliano ya kuondoa kodi kwenye bidhaa za taulo za kike zinazowasitiri wakati wa hedhi yanaendelea ambapo amewasilisha maombi kwa wizara ya fedha na mipango ili kuondolewa katika bajeti ijayo ya fedha.

Waziri ummy amebainisha hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maalum Stella Ikupa ambapo amesema tayari wizara yake imewasilisha ombi hilo ili bidhaa hiyo iunganishwe katika vifaa tiba vilivyo katika msamaha wa kodi.

Amesema kuwa tatizo la gharama na ukosefu wa taulo za hedhi umesababisha idadi kubwa ya wasichana hasa waishio vijijini kukosa masomo yao katika kipindi cha zaidi ya siku tano huku wengine wakitumia nyenzo ambazo sio rafiki katika afya zao.

Kwa upande wake Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtaka mwenyekiti wa wabunge wanawake, Magreth Sitta kuungana na wabunge wabunge wanawake kusimamia kuondolewa kodi katika taulo za usafi za kike ‘pedi’kwani kodi hiyo imekuwa kero.

Kuondolewa kwa kodi kutawezesha kupunguza gharama za taulo hizo, hivyo kuuzwa kwa bei inayokubalika na wengi kumudu kuzinunua.

Post a Comment

0 Comments