Business

header ads

MFANYABIASHARA MANJI AACHIWA HURU KESI UHUJUMU UCHUMIMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka saba ya uhujumu uchumi na Usalama wa Taifa.

Maji na wenzake watatu walioachiwa huru leo Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere walishtakiwa baada ya kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 200 pamoja na mihuri.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amewaachia huru washtakiwa hao mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kisheny Mutalemwa kuomba kesi hiyo ifutwe kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka hayo dhidi yao na Mahakama ikaridhia.

Wakili Mutalemwa amesema kuwa walioamba kuondolewa kwa hati ya wito wa mashtaka na kuiarifu Mahakama kuwa DPP kwa niaba ya Jamhuri hakusudii kuendelea na kesi hiyo na kuomba iondolewe chini ya kifungu cha sheria namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20.

Post a Comment

0 Comments