Business

header ads

BUNGE LAPITISHA MUSWAADA WA SHERIA YA MADAKTARI 2016Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Sheria ya Madaktari ,Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa Mwaka 2016 ili kuhakikisha jamii inapata huduma za tiba nzuri na salama.

Akiwasilisha hotuba ya wizara Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Wazee na Watoto anatoa Maelezo kuhusu Muswada wa Sheria ya Madaktari ,Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa Mwaka 2016 utasaidia kuwasimamia na kuwaongoza wanataaluma wa udaktari katika kuzingatia maadili pamoja na utoaji wa huduma bora za afya.

Waziri Ummy amesema Sheria ya sasa inatoa mamlaka kwa baraza la madaktari kusimamia madaktari na madaktari wa menona kuwaacha , matabibu wasaidizi, wafiziotherapia, wana saikolojia tiba na watengeneza viungo bandia na matabibu wa afya ya akili.

Amesema kuwa sheria inayopendekezwa itaweka mamlaka kwa waziri mwenye dhamana kuteua mwenyekiti huru wa baraza la madaktari kutoka miongoni mwa wanataaluma na kulipa uwezo baraza hilo kujiendesha lenyewe na kuwa na uwezo wa kumiliki mali.

Post a Comment

0 Comments