Business

header ads

UHAMIAJI WMSAFISHA KARIAIdara ya Uhamiaji imetoa ufafanuzi kuhusu uraia wa mgombea wa urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia na kuthibitisha kuwa ni Mtanzania.

Ufafanuzi huo umetolewa na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda ambapo amesema ofisi yake imechunguza na kuthibitisha kuwa Karia alizaliwa nchini na mama yake ni Mtanzania licha ya baba yake kuwa  ni msomali na alikuwa pia na uraia wa Somalia lakini alishaukana.

Mtanda amesema kuwa Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha 5(1) na (2) cha sheria ya uraia wakati huo huo akiwa raia wa Somalia wa kurithi.

Post a Comment

0 Comments