Business

header ads

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MASAMAKI , WENZAKE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Tiagi Masamaki na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7.
Washtakiwa hao wameachiwa huru leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis kuiomba Mahakama iwaachie chini ya kifungi cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya kuendeleza mashtaka yaliyokuwa yakiwakabilia.
Wengine walioachiwa huru pamoja na Masamaki ni Meneja wa Huduma za Ushuru (TRA) Habib Mponyezya, Meneja Msimamizi na ufuatiliaji forodha Burton Mponyezya, Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru ICD Azam, Eliachi Mrema na Meneja wa Azama ICD Ashrafu Khan.
Hata hivyo baada ya kufutwa kesi hiyo na washtakiwa kuachiwa, wenzao ambao ni Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara (TRA) Hamis Omary, Meneja Operesheni za Usalama na Ulinzi ICD Raymond Louis pamoja na Afisa wa Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta TRA Haroun Mpande na wengine wawili walisomewa mashtaka mbalimbali 110.

Post a Comment

0 Comments