Business

header ads

THRDC YALAANI MAUAJI YA POLISI KIBITIMtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania unalaani vikali mauaji ya kutisha ya polisi wawili wa kikosi cha usalama barabarani katika eneo kati ya Bungu na Jaribu katika Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Pwani.

Akitoa tamko hilo leo Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa amesema kuwa kwa kipindi cha miezi miwili wameuwawa maafisa wa polisi 10 Wilayani Kibiti na kuwa hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na hali hiyo.
Olengurumwa amesema kuwa THRDC inatambua jitihada za kukabiliana na hali ambayo Polisi wetu na Jeshi la Ulinzi, miongoni mwa wengine inachukua, kuwa wanaamini kwamba hatua nyingine za kibunifu na za haraka ni muhimu kuchukuliwa wakati huu.

Amesema Ikiwa hatua za upelelezi za kuchunguza majambazi hawa hazitachukuliwa, kuna hatari kubwa kwa usalama wa nchi na raia wake na kuikumbusha serikali kutambua na kuondosha wahalifu wowote ili nchi iendelee kubaki salama.


Olengurumwa ametaja Sababu Zinazosababisha Kujirudia kwa Matukio hayo ni pamoja na kuwepo kwa mazingira magumu ya kufanya kazi kwa maafisa wa polisi kuanzia kuwepo kwa nyumba duni, vifaa na ukosefu wa magari.
Mengine ni Kuwepo kwa uhusiano mbaya kati ya wananchi na Jeshi la Polisi hasa kutokana na vitendo vingine vya kutumia nguvu kupita kiasi ambavyo wakati mwingine hutumiwa vibaya au polisi kunyanyanyasa raia na wakati mwingine huwaua.
Ikumbukwe kwamba uwezo wa Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu hutegemea uhusiano wake na umma.
Amesema kuwa Jeshi la Polisi bado linatumia mbinu za zamani katika ufuatiliaji naufanyaji wa shughuli zake na kuwa wanapaswa kuwa na vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kuchunguza aina zilizopo za silaha za mpinzani katika umbali wa kilomita kadhaa ili kujilinda.
Aidha ametoa wito kwa Serikali kupitia wizara husika inapaswa kuchukulia jambo hili kwa msisitizo mkubwa na kuongeza jitihada zaidi katika kufanya uchunguzi wa kina  ili kutambua wahalifu wa matukio ya mauaji ya polisi na raia ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
“Tunaiomba serikali iruhusu wajumbe na wanachama wetu kufanya maandamano ya amani nchini kote ili kulaani mauaji haya ili sauti za watetezi ziweze kusikika na kuenea sana katika vita dhidi ya mauaji haya” alisema
Amesema ni wakati  sahihi sasa kwa wananchi kujiunga kwa pamoja kufanya juhudi  katika kupambana na matukio mabaya ya namna hii. “Tunaamini kwamba majambazi hawa ni watu wanaoishi na raia wa kawaida mitaani na ili kujua ni mahali gani  au ni nini wanachofanya tunahitaji kufanya kazi ya pamoja  ambayo itakua kamilkifu na watu wote katika kupambana na vita hii.” alisema

Post a Comment

0 Comments