Business

header ads

MAGUFULI AKEMEA TAASISI ZINAZOKIUKA MAADILIRais John Magufuli ameziponda vikali taasisi  zinazohalalisha mapenzi ya jinsia moja na kuhimiza wanafunzi wanaopata mimba shuleni, kurudi shule baada ya kujifungua.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani ambako amezindua barabara ya  Msata – Bagamoyo ambapo amesema ni aibu kwa Watanzania kuiga mambo mbalimbali ambayo ni kinyume cha maadili ya taifa.

“Hawa wageni wanaleta mambo mengine mabaya, wametuletea dawa za kulevya watoto wetu wanatoka kamasi, hawawezi kulima, hawawezi hata  kufanya kazi yoyote, wengine wanatuletea mambo ya ajabu,” amesema na kuongeza;

“Ni ujinga ni upumbavu, Watanzania tujiangalie wanaleta vimichango, lakini kumbe hela zenyewe ni zetu, matokeo yake tunafundishwa michezo ambayo hata ngombe, mbuzi hawawezi kukosea.”

Rais alizitaka  taasisi hizo za kiraia zifungue shule za wazazi badala ya kuilazimisha Serikali kutoa fedha za bure ili waliojifungua warudi shule.


“Hata kama mimi nina mtoto wangu wa kike, aende akapate mimba huko halafu arudi shuleni? Haiwezekani,” amesema.

Post a Comment

0 Comments