Business

header ads

JINSI YA KUPATA WATOTO MAPACHA
Watu wengi sana hupenda kuwa na watoto mapacha, hii huchangiwa sana na jinsi wanavyoonekana mfano wakiwavaa huo za kufanana huvutia mchanoni pa wengi. Licha ya wengi kutamani kuwa na mapacha, ni watu wachache sana ambao hubahatika kuwapata ambapo wengi huihusisha na asili.
Kwa miaka ya nyuma iliaminika kuwa kupata watoto mapacha inawezekana tu kama kwenye familia au ukoo wenu mna asili ya kupata mapacha, kama hamna basi wewe sahau kuwapata.

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia wataalamu wa afya wameweza kuelezea mambo mabali mbali yanayoweza kuchangia mtu yeyote kupata watoto mapacha. Mbali na hilo kuna aina ya wanawake ambao wao wanauwezekano mkubwa sana wa kupata mapacha.

Akielezea mada hii kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dr. Joachim Mabula alisema kuwa kuna aina mbili za mapacha ambazo mwanamke huweza kupata. Aina ya kwanza ya ni mapacha wa wa kufanana ambao hawa hupatikana pale ambapo yai moja la mwanamke hurutubishwa na kisha kugawanyika na kutengeneza watoto wawili. Mapacha hawa wa kufanana mara nyingi sana huwa wa jinsi moja na huwa na tabia zinazoendana sana.

Aina ya pili ya mapacha, ni mapacha wasiofanana. Mapacha hawa hutokea pale ambao mwanamke anatoa mayai mawili ambayo hurutubishwa na mbegu mbili tofauti na mwanaume na hivyo kila yai huu mtoto. Mapacha hawa wanaweza kuwa wa jinsia moja au toauti. Mara nyingine wanaweza wasiwe na tabia za kufanana wakawa kama ndugu waliozaliwa kwa nyakati tofauti. Na aina hii ya mapacha ndiyo maarufu sana duniani.

Juu ni mapacha wa wasiofanana na chini ni mapacha wanaofanana.
Mabula alieleza kuwa mwanamke yeyote anaweza kuzaa mapacha hata kama kwenye familia yao hakuna mtu aliyewahi kuzaa mapacha. Mtaalamu huyo wa afya alisema baadhi ya wanasayansi wanadai mbegu ya kiume ikiwa na nguvu kubwa husababisha kuvunjika kwa yai na kusababisha mapacha.

Aidha alishauri kuwa ili mwanamke kuweza kuwa na mimba yenye afya na kupata matokeo mazuri anayoyahitaji, aache kabisa au apunguze kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya. Lakini pia, ili mwanamke ashike ujauzito kiurahisi tendo la ndoa linapaswa kuwa na maujuzi ili kulifurahia na kupata matokeo mazuri.
“Wenzi wenye matatizo ya kutopata mtoto ambao vipimo vyao havionyeshi tatizo basi wanakosea namna ya kufanya tendo la ndoa,” alisema Dr. Mabula alipokuwa akitoa elimu hiyo kupitia kipindi cha Elimika Wikiendi ambacho hufanyika kila siku ya Jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi kupitia mtandao wa Twitter.
Akielezea aina za wanawake wanaoweza kupata watoto mapacha, Dr. Mabula alisema;
  1. Wanawake wenye asili ya ki-Aafrika mafano wanawake kutokea Nigerai wanapata mapacha mara nyingi.
  2. Mwanamke anayetoka kwenye familia ambayo wanawake wanazaa mapacha.
  3. Wanawake wanaobeba mimba wakiwa na umri mkubwa kuanzia miaka 35 na kuendelea.
  4. Wanawake wanene wa kati na warefu wana uwezekano mkubwa wa kupata mapacha.
  5. Wanawake waliozaa watoto wanne au zaidi wana uwezekano mkubwa wa kupata mapacha.
  6. Wanawake walioharibu mimba wanaweza kupata mimba ya mapacha mbeleni.
Kwa wale ambao wanatamani kupata watoto mapacha, Dr. Mabula alieleza mambo kadhaa ambayo ni muhimu kufanywa na wazazi, ambayo ni pamoja na;
  1. Kutumia bidhaa zinazotokana na maziwa mfano yoghurt na mihogo.
  2. Mwanamke kubeba ujauzito wakati bado ananyonyesha.
  3. Matumizi ya magnesiamu, kalsiamu. Dr. Mabuli alitahadharisha kuwa, matumizi hayo huongeza uwezekano wa kupata mtoto wa jinsia ya kike.
  4. Kupandikiza maabara mbegu za kiume na mayai kisha kuyahamishia kwa mwanamke. Upandikizaji huongeza fursa ya kupata mapacha kwa maana kiinitete zaidi kimoja kinaweza kuhamishwa baada ya kurutubishwa.
Mwanamke anapokuwa na ujauzito wa kati ya kipindi cha wiki 8 hadi 12 kinatosha kutambua kama ujauzito uliobeba una mapacha kwa kutumia ultrasound.

Source: Swahilitimes

Post a Comment

0 Comments