Business

header ads

JESHI LA POLISI NCHINI LATOA TAHADAHARI SIKUKUU YA EID EL FITRIJeshi la Polisi nchini limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El Fitri,

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na msemaji wa jeshi hilo nchini Advera Bulimba amesema kuwa kipindi cha sikukuu baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu na vitendo vingine ambavyo huhatarisha usalama wa watu na mali zao.

Bulimba amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhakikisha kwambawananchi wanasherehekea sikukuu katika hali ya amani na utulivu.

Amesema ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo yakuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayoyatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Aidha Jeshi la Polisi linawatahadharisha watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kuwa makini na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani,na kuwa jeshi hilo halitasita kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaovunjasheria na kanuni za usalama barabarani.

“Madereva kutumia vilevi,bodaboda kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi pamoja na kupiga honi hovyo. Watachukuliwa hatua”

Pia, amewataka wananchi wote kuwa wepesi katika kutoa taarifa kwa kupitianamba za simu za bure au pindi wanapoona viashiria vyovyote vyauhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara.

Post a Comment

0 Comments