Business

header ads

BEI YA MAFUTA YASHUKA KWA ASILIMIA 1

 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ya petroli ambayo imeshuka kwa asilimia moja ukilinganisha na bei iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.

Akitangaza bei hizo leo Jjini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA Bw. Titus Kaguo amesema kuanzia Julai Moshi , bei hizo zitashuka na kuuzwa kwa Sh37 kwa lita (sawa na asilimia 1.81 wakati dizeli itauzwa kwa Sh 14 kwa lita (0.73 asilimia). Mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 19 kwa lita (sawa na asilimia 1.03)


Kwa bei za jumla, mafuta ya petroli yamepungua na sasa yanauzwa kwa Sh 37.21 kwa lita(sawa na asilimia 1.92)na dizeli itauzwa kwa Sh 13.70 kwa lita(sawa na asilimia 0.77) na mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 18.85 (sawa  asilimia 1.10)

Post a Comment

0 Comments