Business

header ads

WATU 33 WAFARIKI AJALI YA BASI KARATU ARUSHA
Watu 33 wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya coaster yenye namba za usajili T781 DYX  iliyokuwa ikisafirisha wanafunzi wa shule ya msingi kutoka Lucky Vincent  ya Arusha ambao walikuwa wakienda kufanya mtihani wa ujirani mwema katika shule Tumaini junior School iliyopo Wilayani Karatu mkoani Arusha.

Akithibistisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo amesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kuacha njia na kuingia katika bonde la mto Mlera ambapo maiti wamepelekwa katika Hospital ya Lutheran Karatu gari likiwa na abiria 38.

Amesema kuwa wanafunzi 30 wamefariki hapo hapo na wengine watu wazima 3 kati yao akiwemo ni dereva na majeruni watano ambao wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Arusha.

Post a Comment

0 Comments