Business

header ads

WANAWAKE WATAKIWA KUWEZESHWA KIUCHUMI


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mhe Ummy Mwalimu amesema Ili kufikia Tanzania ya viwanda nchi inahitaji kuongeza kasi ya kuhakikisha wanawake wanawezeshwa kiuchumi, wanashiriki katika ajira na kukomesha vitendo vyote vya ukatili dhidi yao.
Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoani Singida ambapo amesema katika kutekeleza kaulimbiu ya Tanzania ya viwanda Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi na ni lazma kuwekeza katika shughuli zitakazowezesha Ushiriki kamili wa wanawake katika shughuli za kiuchumi.

Aidha Waziri Ummy, ameiagiza Halmashauri ya Singida Manispaa kutoa asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kabla ya mwaka wa fedha 2016/2017 kuisha pamoja na kuahidi kufungua dirisha la Benki ya Wanawake katika Mkoa wa Singida ndani ya miezi sita ijayo.
Amesema kuwa haki ya mtoto wa kike ni kusoma sio kuolewa na kuongeza kuwa nchi haiwezi kujenga uchumi wa Tanzania ya viwanda ikiwa asilimia 37 ya watoto wameolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. “hatuwezi kujenga Tanzania ya viwanda ikiwa asilimia 27 ya watoto wa Tanzania wana watoto”

Pia Mhe Ummy amewataka wananchi wa Mkoa wa Singida kuachana na Mila na desturi ya kukeketa watoto wa kike. Aliwasihi wananchi waliohudhulia hadhara hiyo kwenda kuelimisha na kuhamasisha umma wa Singida kuacha vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike.Post a Comment

0 Comments