Business

header ads

WATUHUMIWA 257 WAKAMATWA MSAKO WA DAWA ZA KULEVYA DAR


 Jeshi ya Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limesema mpaka sasa wamefanikiwa kukamata jumla watuhumiwa 257 pamoja na ya kete za dawa za kulevya 1,526 puli 112 na misokoto ya bangi 247
 
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro Kamishna Sirro ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya ahabari ambapo amesema wapo watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao hawajafikishwa mahakamani kwa sababu upelelezi haujakamilika.

Aidha Kamanda Sirro amesema kuanzia February 18-23 mwaka huu Jeshi la Polisi usalama barabarani wamefanuikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 460 kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani pamoja na kukamata pikipiki 1,280 kati ya hizo pikipiki 30 zimekamatwa kutokana na kupita katika njia ya mabasi yaendayo haraka.

Post a Comment

0 Comments