Business

header ads

WAANDISHI WASIO NA STASHAHADA HAWATORUHUSIWA KUANDIKA HABARISerikali imetoa kipindi cha mpito cha miaka mitano kwa wanahabari walioko kazini ambao hawana kiwango cha chini cha elimu ya Stashada, kusoma ili kufikia kiwango hicho.

Kabla ya kutolewa kwa kanuni hiyo, kulikuwa na mjadala mzito ndani na nje ya tasnia ya habari, baadhi wakitaka kiwango cha chini cha elimu ya mwanahabari kiwe ni shahada ya kwanza.

Taarifa hiyo ilitolewa mjini Dodoma jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati akitangaza kuanza kutumika kwa sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za 2017.

Hata hivyo, Waziri Nape alisema ili kusaidia wanahabari waliopo kazini waweze kujiendeleza, Serikali kupitia Idara ya Habari, itaendelea kutoa vitambulisho (Press Card) bila kuwabana sana wanahabari.
Tutaendelea kutoa Press Card bila kuwabana sana wanahabari kwa kuangalia vigezo hivi vya kitaaluma bali dhamana ya waajiri wao,” alisema na kusisitiza ambao hawana Stashahada wakasome.

Alisema wakati wa kuandaa kanuni hizo, wizara yake ilipokea maoni ya wadau wengi na baadhi yao walitaka mwandishi wa habari awe na elimu ya cheti, wengine stashahada na shahada ya kwanza.

Kuna ambao walitaka iwe hata PhD (shahada ya udaktari) na wapo waliotaka iwe mtu anayejua kusoma na kuandika. Serikali imesimama katikati ya maoni hayo na kuja na Diploma,”alisema.
Alisema kanuni hizo zimesheheni masuala ya kusaidia utekelezaji wa sheria hasa muktadha mzima wa kuifanya nchi iwe na vyombo vya habari vyenye uhuru wa kutosha na vinavyowajibika kwa umma.
Katika kutekeleza sheria hiyo, Nape alisema zipo taasisi ambazo zipo kama Idara ya Habari ambazo zitaongezewa majukumu au kazi zake kuhuishwa na kuna vyombo vipya vitaanzishwa.
Umma na wanahabari wanakumbushwa kuwa sheria hii, imeweka wajibu kwa wale watakaokiuka misingi na maadili ya taaluma hii. Ukurasa mpya wa haki na wajibu umefunguliwa,” alisema.
Alisema sheria hiyo inaleta mfumo madhubuti wa kulinda haki za wanahabari kukusanya, kuhariri na kusambaza habari kwa uhuru na vyombo vyao sasa vitatekeleza haki hiyo ya kikatiba bila vikwazo.
Kwa mujibu wa Waziri Nape, sheria ya huduma za vyombo vya habari ya mwaka 2016 ilianza kutumika rasmi Desemba 31,2016 wakati kanuni hizo za 2017 zimeanza kutumika Februari 3,2017.
Akijibu swali la mwandishi mwandamizi wa Mtanzania, Paul Maregesi kuhusu kiwango cha chini cha Mhariri, Waziri Nape alisema Serikali imeamua isijiingize kupanga kiwango cha elimu cha mhariri.
Chini ya sheria hiyo, mwandishi au mtu yeyote atakayetumia chombo cha habari kutoa taarifa za uongo zinazotishia usalama, kuchafua au kuchafua sifa za mtu mwingine anatenda kosa la jinai.
Kulingana na sheria hiyo, mtu huyo akipatikana na hatia atahukumiwa kulipa faini isiyopungua Sh5 milioni lakini isiyozidi Sh20 milioni au kifungo cha hadi miaka mitano jela au vyote viwili.
SOURCE:mwananchi

Post a Comment

0 Comments