Business

header ads

VIONGOZI WA UPINZANI KENYA WAUNGANA

Viongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, NASA, wamesaini makubaliano ya kugawana madaraka ambayo yatawaunganisha dhidi ya chama tawala cha Jubilee katika uchaguzi mkuu ujao.

Makubaliano hayo yanashirikisha mapendekezo ya kubuniwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu ambao kulingana na duru za chama hicho atateuliwa mgombea atakayeibuka wa tatu katika mchujo wa uteuzi wa mgombea wa Urais.

Duru katika mkutano huo zinasema mgombea atakayeshinda uteuzi huo atapeperusha bendera ya chama hicho huku mgombea atakayeibuka katika nafasi ya pili akichukua wadhifa wa Naibu wa Rais.


Viongozi wakuu wa muungano huo ni Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga (ODM), Makamu wa Rais wa Zamani, Kalonzo Musyoka, (WDM), Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje, Moses Wetangula, ( Fkenya), na Naibu Waziri Mkuu wa zamani Musalia Mudavadi, (ANC).

Post a Comment

0 Comments