Business

header ads

NUKUU ZA RAIS DKT. MAGUFULU LEO FEB 06, 2017


“Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni”

“Najua IGP kuna watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu dawa za kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa ni IGP”

“Haiwezekani vijana tunaotarajia kupawa nchi kesho wanatumia dawa alafu kuna watu wanapita na kutamba kwa utaji”

“IGP nakuagiza kamata watuamiaji wote wa dawa za kulevya hao watakwambia wanapozipata, haiwezekani ziuzwe kama njugu”

“Vita ya dawa za kulevya si ya Paul Makonda peke yake, ni ya watanzania wote, naviagiza vyombo vyote vishirikiane”

“Kuna mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa mahakamani”

“Sikutaka kumchagua Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kabla sijaenda Ethiopia sababu nilijua watasema Mwamunyange ametumbuliwa”

“Nataka wafungwa wawe wanafanyakazi, ukiwafunga tu na kuwapa chakula ndio sababu wanarudia makosa kila siku wakitoka”

“Ombi langu ni Tanzania ya viwanda ionekane kwenye majeshi yetu, haiwezekani hadi leo tunaagiza sare kutoka nje ya nchi”

Baadhi ya Nukuu za Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hotuba yake wakati wa kumuapisha Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments