Business

header ads

MFUMUKO WA BEI WAPANDA KWA ASILIMIA 0.2
Kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimeongezeka kutoka asilimia 5 ilivyokuwa mwezi Disemba mwaka jana hadi asilimia 5. 2 hii ikiwa ni ishara kwamba kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma imeongezeka kwa wastani wa asilimia 0.2.Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo na kutaja sababu ya ongezeko hilo kuwa ni kupanda kwa takribani bidhaa na huduma zote ambazo hutumika kupima mfumuko wa bei.Kwa mujibu wa Bw. Kwesigabo, kasi ya mfumuko wa bei nchini ni ndogo ikilinganishwa na nchi za jirani za Uganda na Kenya na kwamba thamani ya shilingi mia moja katika manunuzi ya bidhaa na huduma imefikia shilingi 94 na senti 42 kutoka shilingi 95 na senti 20 ilivyokuwa mwezi Disemba."Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari 2017 kutoka 1-05.04 mwezi Desemba 2016" alisema Kwesigabo.Alisema kuongeza kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.Alitaja baadhi za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia 6.3, ndizi za kupika kwa asilimia 5.8, magimbi kwa asilimia 5.3 na viazi vitamu kwa asilimia 6.5.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilichochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mkaa kwa asilimia 3.2 na majokofu kwa asilimia 2.4.Kwesigabo alisema thamani ya shilingi ya Tanzania hupima badiliko la uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo shilingi ya Tanzania ingeweza kununua katikavipindi tofauti.

"Ikiwa fahirisi za bei za Taifa zinaongezeka, uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma hupungua" alisema Kwesigabo.Alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 94 na senti 42 mwezi Januari, 2017 ikilinganisha na shilingi 95 na senti 20 ilivyokuewa mwezi Desemba 2016.

Post a Comment

0 Comments