Business

header ads

MAHAKAMA YA KISUTU YATOA HAKI YA DHAMANA WATUHUMIWA DAWA ZA KULEVYA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imetoa dhamana kwa baadhi ya wasanii waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.Dhamana hiyo imetolewa na Mahakimu wawili mahakamani hapo, ambapo katika shauri la kwanza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia ombi lililowasilishwa Mahakamani hapo na upande wa Jamuhuri la kuwataka watuhumiwa 5 wa dawa za kulevya kuwa chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kwa kipindi cha miaka 3 na kuwasilisha dhamana ya shilingi milioni 20 pamoja na mdhamini mmoja na kisha kuachiwa huru.

Hakimu Mkazi Cyprian Mkeha ametoa dhamana hiyo kwa wasanii watano akiwemo, Ahmed Hashim aka Petitman, Lulu Abbas Chelangwa aka Luludiva na Said Masoud aka Said Alteza na wengine wawili ambao kwa pamoja wataachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini moja kwa dhamana ya kiasi cha shilingi milioni 20.

Katika Dhamana ya pili iliyotolewa na Hahimu mwingine ambaye ni Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Saidi kwa watuhumiwa 8 ambao ni pamoja na Rommy Jones, Khalid Mohamed aka TID, Babu wa Kitaa, Mwana dada Tunda, Joan, Rachel na wengine, Mahakama imeridhia ombi la Jamuhuri na kuwataka kutoa dhamana ya Shilingi Milioni 10, na kufika kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi kwa muda wa mwaka mmoja.

Awali jeshi la polisi liliwasilisha ombi hilo Mahakamani hapo kutaka watuhumiwa hao kusomewa kiapo cha Mahakama ili waweze kuwa chini ya uangalizi kubaini kama wameachana na tabia hizo za utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwa raia wema.


Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amethibitisha kwamba, wanamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kufuatia kauli zake alizozitoa dhidi ya serikali.

Mh. Lissu alikamatwa jana jioni mjini Dodoma baada ya kutoka kwenye kikao cha Bunge na kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam.


Post a Comment

0 Comments