Business

header ads

MAHAKAMA KUU YATOA ZUIO DHIDI YA MBOWE

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo imetoa zuio la muda hadi Ijumaa kwa Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe asikamatwe na vyombo vya dola hadi hapo kesi yake ya msingi ya pingamizi aliyoifungua itakaposikilizwa.

Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na kumpa ahueni Mhe. Mbowe ambaye jana jioni alishikiliwa na polisi kwa muda hadi usiku wa manane na kuhojiwa, ambapo sasa kwa uamuzi wa Mahakama polisi wanaruhusiwa kumhoji tu lakini si kumkamata.
 
Mahakama Kuu pia imetoa ruhusa kwa mleta maombi Mhe. Mbowe kurekebisha maombi aliyoleta Mahakamani ili kumuingiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika shauri hilo pamoja na kufanya marekebisho mengine madogo madogo ambayo wataona yanafaa katika shauri hilo.
 
Februari 10 mwaka huu, Mhe. Mbowe alifungua shauri la Kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam.
Katika shauri namba 1 la 2017, Mhe. Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha na kukamata. Pia ameiomba Mahakama itengue vifungu namba 5 na 7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki za Kikatiba.


Post a Comment

0 Comments