Business

header ads

Jumla ya kete 299 za dawa za kulevya zimekamatwa na Jeshi la PolisiJumla ya kete 299 za dawa za kulevya zimekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kufanyika msako kwenye nyumba za watuhumiwa 112 wa dawa za kulevya wanaoshikiliwa na jeshi hilo kwa muda wa siku 3 ambapo 12 kati yao tayari wamefikishwa Mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu waliokamatwa wakijiusisha na dawa za kulevya Kamanda Sirro amesema, watuhumiwa 12 akiwemo muigizaji filamu Wema Sepetu wamesomewa mashtaka yao mara baada ya kukiri kutumia dawa za kulevya na kukutwa na vielelezo na kwamba watuhumiwa wengine 100 watafikishwa Mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika..

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Poul Makonda ametoa siku 10 kwa watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya kujisalimisha katika kituo cha Polisi Kati, sambamba na kuwataka Wenyeviti wa Serizali za Mitaa kuwasilisha orodha ya wakazi wao wanajihusisha na matumizi na biashara ya dawa za kulevya...

Akitoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam, Mhe. Makonda amesema, muda wa siku 10 alioutoa utawahusu Wenyeviti wa serikali za mitaa wote katika Mkoa wake, Wazazi wenye watoto wanaojihusha na dawa ya kulevya na watumiaji wenyewe kujisalimisha kwani oparesheni ya kumaliza matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya Jijini Dar es Salaam, inaendelea.

Post a Comment

0 Comments