Business

header ads

JESHI LA POLISI LAWASIMAMISHA KAZI ASKARI 12 WALIOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYAMkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi Askari 12 waliotuhumiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kupisha uchunguzi ufanyike dhidi yao.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam IGP Mangu amesema ni lazima Jeshi la polisi lichukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, bila kuangalia cheo chake na hata kama ni Askari.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi linachukua hatua madhubuti za kuwachunguza Askari na Wasanii wote waliotuhumiwa na baada ya uchunguzi kumamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethibitika kwa uhalifu huo.

Aidha IGP Mangu ameiomba jamii kuendelea kutoa taarifa za uhalifu wa aina yeyote ili nchi iendelee kuwa salama. Hapo chini ni Majina ya Askari wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya, ambao wamesimamishwa kazi.

Uamuzi huo unafanyika Kufuatia tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda zikiwahusisha baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Post a Comment

0 Comments