Business

header ads

KAULI ZA MAALIM SEIF KATIKA MAHOJIANO


Baadhi ya kauli alizotoa Katibu Mkuu wa chama cha  CUF Zanzibar, Maalim Seif Sharifu Hamadi katika mahojiano yake katika kipindi cha Funguka na Tido Mhando.
Mimi ni mtu wa misingi, hakuna sehemu Katiba inasema kurudia uchaguzi, ulirudiwa kwa misingi ipi?
Hivi sasa dunia haikubali mtu kung'ang'ania madaraka hata kama umeshindwa, hili linaendelea kufuatiliwa.

Iwapo mahakama itakubaliana na hoja za msajili kuhusu Prof Lipumba, tutaheshimu maamuzi.

Sijapata hata kufikiria kuunda chama wala kufikiria kujiunga na chama kingine

Katiba yetu inasema mtu akijiuzulu wadhifa wake, hana nafasi ya kurudi tena

Natarajia baada ya muda mfupi ujao nitakuwa rais wa Zanzibar.

Baada ya kuacha wadhifa safari zote za nje najilipia mwenyewe na siombi serikalini ingawa nina haki'-Maalim Seif 

Jimbo la Dimani kihistoria ni la CCM na sisi tuliingia kwenye uchaguzi tukijua tuna kazi kubwa'-Maalim Seif

Post a Comment

0 Comments