Business

header ads

IDADI YA WALIOFUKIWA GEITA YAFIKIA 15,WAOMBA CHAKULA


Juhudi za kuwatafuta wachimbaji wadogo zimeonyesha dalili nzuri baada ya kufahamika kuwa wapo hai, baada ya kutuma ujumbe uliotaja majina yao na idadi kwamba wako 15, tofauti na 14 kama ilivyokuwa ikiripotiwa awali.
Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Nishati, Medadi Kalemani, mmoja wa watu waliopo katika timu ya uokoaji, Felix Adolf alisema licha ya maombi hayo, ilishauriwa kuwa watu hao waliofukiwa watumiwe maji ya glucose yanayochanganywa na timu ya madaktari iliyopo hapo.
Wachimbaji hao waliofukiwa na kifusi cha udongo kwa zaidi ya siku tatu sasa katika Mgodi wa RZ mkoani Geita, wamekuwa wakiwasiliana kwa kutumia bomba la kuchimbia maji.
Katibu wa wachimbaji wadogo katika Mkoa wa Geita, Golden Hainga alisema jana kuwa kazi ya kuchimba ili kuingiza bomba la kuwapelekea maji na chakula wachimbaji hao walioko chini, ilifanikiwa na waligonga bomba hilo kuashiria kuwa wako hai.
SOURCE:MWANANCHI

Post a Comment

0 Comments