Business

header ads

HOTUBA YA MWISHO YA RAIS OBAMA CHICAGO MAREKANI
Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia, wakati akitoa hotuba yake ya mwisho kama rais wa Marekani mjini Chicago.
Obama alisema Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka nane iliyopita alipochukua madaraka.
Aidha amewaomba Wamarekani wa kila asili kuangazia mambo kutoka kwa msimamo wa wengine, na kusema kwamba lazima tuwategee sikio wengine na kusikia
Alisema utamaduni wa kukabidhi madaraka kwa warithi kwa njia ya amani ni moja ya mambo makuu yanayotambuliwa katika demokrasia Marekani.
Hata hivyo amesema kuna mambo matatu yanayotishia demokrasia Marekani yakiwemo ukosefu wa usawa kiuchumi, mgawanyiko kwa misingi ya rangi na hatua ya baadhi ya makundi kwenye jamii kujitenga na kuwa na misimamo ambayo haiongozwi na ukweli.

Post a Comment

0 Comments