Business

header ads

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUFUNGUA KESI
Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania wameazimia kufungua kesi 7 katika mahakama ya Afrika Mashariki wakiitaka baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na mkataba wa kusimamia haki za binadamu ambao kwa sasa wamedai katika mkataba huo hakuna kipengele hicho cha sheria.

Mkurugenzi wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania Bw. Onesmo Olengurumwa amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akitoa maazimio ya mkutano wa watetezi wa haki za binadamu uliofanyika jijini Dar es salaam kwa siku mbili.

Amesema katika mkutano huo, Wamekubaliana kufungua kesi katika mahakama hiyo ya Afrika Mashariki ili kupinga hatua ya serikali ya Tanzania kuzuia matangazo ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuonyesha moja kwa moja kupitia runinga na kesi nyingine 6 ambazo wamedai kuwa zinakiuka misingi ya haki za binadamu hasa uhuru wa kujieleza…

Naye Mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka taasisi ya Vijana ya TYVA Bi. Zuleha Ibrahim amesema hapo awali awakuwa na uelewa wa kujua namna ya kufungua kesi katika Mahakama hiyo na kwamba baada ya mkutano huo kwa pamoja wamekubaliana kufungua kesi hizo..

Post a Comment

0 Comments