Business

header ads

RAIS MAGUFULI ACHANGIA MIL 5 KWA MTOTO HAIDARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wametoa mchango wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto Haidari Bonge anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama kichwani, mdomoni na machoni.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 7, anaishi Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam na alianza kupata tatizo la kuota nyama miezi mitatu baada ya kuzaliwa na amekuwa akifanyiwa upasuaji wa kuondoa nyama hizo mara kwa mara.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia vyombo vya habari, Rais Magufuli amesema yeye na mke wake wameguswa na tatizo linalomkabili mtoto Hidari na kwamba wameamua kuchangia shilingi milioni 5 kutoka kwenye mshahara wake kwa ajili ya kuchangia matibabu ya mtoto huyo.

Aidha, Rais Magufuli amesema wanatoa pole kwake na kwa familia yake ambayo imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuhakikisha anapatiwa matibabu kwa kipindi kirefu cha miaka 7 sasa.

Post a Comment

0 Comments