Business

header ads

MAKAMU WA RAIS AHIMIZA WATU KUFANYA MAZOEZI KUEPUKA MAGONJWA

Makamu wa Rais, Mh. Samia Hassan Suluhu (katikati), Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dkt. Hamis Kigwangala (kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakiwa katika kampeni ya kufanya mazoezi katika viwanj vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametangaza kwamba kuanzia sasa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa ni siku ya kitaifa ya mazoezi kwa afya ikiwa ni katika jitihada za kuwataka wananchi kushiriki kufanya mazoezi ili kuepukana magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza na amewataka wakuu wa mikoa, wilaya zote hapa nchini kuweka utaratibu kufanya mazoezi na kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu.

Amesema anafahamu kuna tatizo kwenye Halmashauri mbalimbali kuwa  wameuza   viwanja vya wazi na kuwaagiza  watendaji wa Halmashauri  ndani ya miezi mitatu kuvirudisha viwanja hivyo kwa ajili ya mazoezi hata kama wakishindwa wametakiwa kutangaza maeneo mengie ili wananchi wayatumie kufanya  mazoezi.

Kwa upande wake waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia kwa asilimia 27 ya vifo vyote duniani Ikiwemo Tanzania ambapo idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu endapo hakutakuwa na jitihada mahsusi za kupambana na magonjwa hayo.


Kwa upande wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Dk. Ali Hassan Mwinyi, amewataka watanzania kupenda kufanya mazoezi kwani njia hiyo itawasaidia katika kuongeza siku za kuishi na kufanikiwa kujikinga na magonjwa mbali  mbali. "Nawaambia siri ya umri wangu  ufanyaji mazoezi kwani mimi kila siku natenga dakiki 90 za kufanya mazoezi kila nikiamka’amesema Rais Mstaafu".alisema  Mzee Mwinyi.

Post a Comment

0 Comments