Business

header ads

HALMASHAURI KUU CCM YAFANYA MABADILIKO KUONGEZA UFANISIMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na  Katibu Mkuu  wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufunguliwa rasmi  leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.

Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM imefanya mabadiliko mbalimbali katika chama hicho baada ya kukutana kwaajili ya kupokea taarifa ya tathimini ya chama hicho kuhusu uchaguzi mkuu ulipita pamoja na kutoa mapendekezo juu ya thamini hiyo lengo likiwa ni kuongeza ufanisi ndani na nje ya chama hicho.

Akitoa taarifa ya mapendekezo ya chama hicho katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kuwa baada ya kutafakari kwa kina taarifa hiyo halmashauri kuu imeamua kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao vya maamuzi ya chama pamoja na idadi ya vikao vya chama kutoka wajumbe 388 hadi kufikia 158

Amesema kwa upande wa vikao vya halmashauri kuu ya taifa kufanyika baada ya miezi sita badala ya miezi minnee ya awali pamoja na NEC kukutana mara mbili badala ya mara tatu ikiwemo kupunguza idadi ya wajumbe kutoka 34 hadi 24.

Ameongeza kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na halmashauri kuu imewateuwa wajumbe wapya ambao watachukua nafasi zilizoachwa wazi baada ya wajumbe waliokuwepo kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za kiserikali ambapo amesema wamemteua

Akiwataja waliochukua nafasi kuwa ni pamoja na Rodrick Mpogoro ambaye amekuwa naibu katibu mkuu wa CCM tanzania bara, Kanali Ngemela Lubinga kuwa katibu wa halmashauri anayeshughulikia siasa na uhusiano wa kimataifa pamoja na Humfrey Polepole ameteuliwa kuwa katibu wa NEC itikadi na uenezi kujaza nafasi iliyoachwa na Nape Nnauye ambaye ni Waziri kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments