Business

header ads

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASISITIZA UPATIKANAJI WA UMEME WA UHAKIKA DAR

Waziri mkuu Mhe Kassim Majaliwa amezindua mradi wa kuboresha upatikanaji wa umeme katika jiji la dar es salaam na kusema kuanzia sasa hakutakuwa kuwa na tatizo la kukatika katika  wala mgao wa umeme  hatua itakayotoa fursa kwa wananchi kuanza kufanyashughuli za uzalishaji mali na kuongeza kipato kutokana na upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, mhe majaliwa amesema serikali ya awamu ya tano ni imara inayoahidi na Kutekeleza na kusisitiza kupitia mradi huo  utafungua fursa za uzalishaji na kupeleka ajira za uhakika kwa wananchi hatua Ambayo itakamilisha azma ya serikali ya awamu ya tano inayozingatia uchumi wa viwandea katika kuelekea kwenye nchi za kipatao cha kati ifikapo mwaka 2025.
Aidha, Mhe Majaliwa amesema serikali imetenga shilingi trilioni 1 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme katika vijiji elfu Nane, kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini-REA- ili kuwawezesha wananchi waishio vijijini kutumia fursa ya umeme katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia gharama za kuvuta umeme ili kuhakikisha lengo la asilimia 75 ya Watanzania kuwa na huduma ya umeme ifikapo mwaka 2025 linafikiwa.
Awali akimkaribisha waziri mkuu, waziri wa nishati na madini Mhe Prof. Sospeter Mhongo amelitaka shirika la umeme nchni- TANESCO- kuhakikisha hakutakuwa na tatizo la kukatika katika kwa umeme katika jiji la Dar es Salaam ili kuwezesha ujenzi wa Nchi kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme nchi Mhandisi Filchesm Mramba  amesema jumla ya shilingi bilioni 74.6 zimetumika kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo wa kuboresha upatikanaji wa umeme katika jiji la Dar es Salaam ambapo kati ya fedha hizo Serikali ya Finland imetoa msaada wa Euro milioni 63.7 sawa na shilingi bilioni 63.5 za Tanzania na serikali ya Tanzania Imechangia dola milioni 5.05 sawa na shilingi bilioni 11.03.

Post a Comment

0 Comments