Business

header ads

WATUHUMIWA SITA WA UHUJUMU UCHUMI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

 

Watu sita wanaodaiwa kuwa vinara wa mtandao wa kukusanya kuuza vipande vya meno ya tembo akiwemo Yusuph Ali Yusumbu marufu kama Mpemba wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jana jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka manne ya kuhujumu uchumi baada ya kukutwa na pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 783.
 
Washtakiwa hao walifikishwa mbele ya hakimu mkazi Thomas Simba na kusomewa mashtaka hayo na mwendesha mashataka wa serikali Paul Kadushi. 
Kadushi aliambia mahakama kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa manne ambapo kwa nyakati na sehemu tofauti katika mikoa ya Dar es Salaama, Morogoro, Iringa, Tanga na Mtwara wakiwa na mtu mwingine ambaye hakuwepo mahakamani hapo walikutwa na pembe za ndovu mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika shtaka la kwanza mwendesha mashtaka huyo alisema kati ya January 2014 na October 2016 washtakiwa hao walikutwa na pambe za Ndovu 50 vyenye thamani ya shilingi milioni 392,817,600 na kuongeza kuwa katika shitaka la pili October 26 mwaka huu huko Mbagala, Zakhem jijini Dar es Salaam washitakiwa walikutwa na vipande 10 vya maeno ya tembo vyenye thamani ya shilingi milioni 65.4.
Mahakama ikaendelea kuambiwa kuwa shtaka la tatu October 27 mwaka huu huko Tabata Kisukulu washtakiwa hao walikutwa na kilo 11.1 zenye thamani ya shilingi milioni 32,734,800. Na katika shtaka la mwisho mahakama imeambiwa kuwa October 29 mwaka huu huko Tabata Kisukulu Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walikutwa na vipande 36 vya pembe za Ndovu vyenye thamani ya uzito wa gramu 58.55 vyenye thamani ya shilingi milioni 294,613,200.

Kadushi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba jamhuri inaandaa nyaraka mbalimbali ikiwemo maelezo ya mashahidi pamoja na vielelezo kwaajili ya kufikishwa katika mahakama maalumu ya kesi za kuhujumu uchumi na Rushwa. 
Kesi hiyo itatajwa tena Desemba mosi na washitakiwa kurudishwa mahabusu.

Post a Comment

0 Comments