Business

header ads

WALIOGHUSHI VYETI KUPATA MIKOPO KUKIONAWaziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa baada ya uhakiki wa vyeti vya vifo vilivyowasilishwa na wanafunzi wanaoomba mikopo wakidai kwamba ni yatima, watakaobainika kupeleka vyeti vilivyoghushiwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa elimu jana Dar es Salaam, Profesa Ndalichako alisema kwa wanafunzi ambao wanatambua kwamba walipeleka vyeti feki vya vifo na ripoti za daktari kuonesha kwamba wana magonjwa mbalimbali ambayo wanastahili kupewa mkopo, wajisalimishe kuepuka usumbufu watakaoupata.

Aidha, alisema timu ya kukagua vyuo vyote nchini ikikamilisha ripoti yake vyuo ambavyo havitastahili kutoa kozi fulani au kutoa mafunzo yote, vitafungiwa.

Alisema baada ya vyuo hivyo kufungwa serikali itachukua jukumu la kuwapeleka wanafunzi katika vyuo vingine ili kuendelea na masomo yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) hivi karibuni kubaini uwepo wa baadhi ya wanafunzi ambao wamewasilisha vyeti feki vya vifo vya wazazi wao ili waonekane kama ni watoto yatima, huku wakihitaji kupewa kipaumbele cha kupatiwa mkopo.

Post a Comment

0 Comments