Business

header ads

WADAIWA SUGU WA MIKOPO KUPELEKWA MAHAKAMANI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB) imesema itawachukulia hatua kali ikiwemo kuwafikisha mahakamani wanufaika sugu 142,470 wa mikopo ambao hawajatoa wala kuanza kuanza kurejesha mikopo yao yenye thamani ya shilingi  239, 351,750, 176.27.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Bw. Abdul-Razaq Badru ambapo amesema wametoa notisi ya siku 30 kuanzia leo wadaiwa hao wawe wamekwishalipa kiasi chote cha mkopo wanachodaiwa pamoja na kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani watakaokaidi ili walipe madeni yao na gharama za kuwatafuta pamoja na kuendesha kesi. 
Aidha amesema  Jumla ya wanufaika wa mikopo 93,500 wamebainika na kupelekewa ankara za madeni yao, kati ya hao wanufaika 81,055 wameendelea kulipa mikopo yao,wanufaika 12, 445 hawajaanza kulipa.

Post a Comment

0 Comments