Business

header ads

UWEZO WA SHILINGI WASHUKA
Mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba mwaka huu umebaki kiwango kile kile kilichokuwa mwezi Septemba, ambapo kasi ya kupanda kwa bei ya bidhaa na gharama za huduma imebakia katika kiwango cha asilimia nne nukta tano.
Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja, amewaambia wanahabari jijini Dar es Salaam leo kuwa uwezo wa shilingi katika manunuzi umeshuka na kufikia shilingi 96 na senti 92 ikilinganishwa na shilingi 97 na senti 04 hapo mwezi Septemba.


Mtakwimu huyo amefafanua Kuwa mfumuko wa bei Kwa mwezi Octoba 2016 imechangiwa na kuongezeka Kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa Za vyakula na zisizo Za vyakula kipindi kilicho ishia mwezi Oktoba 2016  zikilinganishwa na bei Za mwezi Octoba 2015 ambapo Mwenendo wa bidhaa Za vyakula zilizoonesha kuongezeka ni pamoja na mahindi Kwa asilimia 18.3, unga wa ngano Kwa asilimia 4.8, samaki wa bichi Kwa 5.07, ndizi za kupika Kwa asilimia 5.2.
Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula  kama Mkaa umeongezeka Kwa asilimia 15.4 na vyakula kwenye migahawa vimeongezeka Kwa asilimia 17.3.
Minja ameongeza Kuwa fahirisi Za bei zimeongeka Hadi asilimia 103.17 mwezi Oktoba 2016 kutoka 103.05 mwezi September 2016 kuongezeka Kwa fahilisi Za bei kumechangiwa na kuongezeka Kwa bei Za baadhi ya bidhaa Za vyakula na bidhaa zisizo Za vyakula bidha Za vyakula zilizo changia kuongezeka Ni samaki wa bichi Kwa asilimia 9.8. Mihogo Kwa asilimia 9.7, mahindi Kwa asilimia 4.7 Katanga Kwa asilimia 3.7, maharage Kwa asilimia 3.8. Huku Kwa bidhaa zisizo Za vyakula fahilisi zilizo ongezeka Ni gharama ya kodi ya pango Kwaajili ya makazi Kwa asilimia 2.9 na Mkaa Kwa asilimia 1.1,

Post a Comment

0 Comments