Business

header ads

SERIKALI YAANISHA MPANGO WA MAENDELEO 2017/2018
Serikali imeainisha maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2017/2018 kulingana na mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka ujao wa fedha.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.

Dk. Mpango amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na miradi ya kielelezo ya maendeleo ambayo inayolenga kufanikisha utekelezaji wa Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

Ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na Makaa ya Mawe Mchuchuma, Mchuchuma Liganga, ujenzi wa reli ya kati kutoka Dar es salaam, Tabora hadi Kigoma yenye urefu wa km 1,251 kwa “Standard Gauge” pamoja na matawi yake yote.

Dk. Mpango ameyataja maeneo mengine ya kipaumbele kuwa ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa kukuza uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo y uchumi na maendeleo ya watu, mazingira ya wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji, ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na maeneo mengine muhimu kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa taifa.

Aidha Dkt. Mpango amesisitiza uwepo usimamizi na udhibiti wa matumizi, ulipaji na ongezeko la madeni ya Serikali, ukusanyaji wa mapato pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za utekelezaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Hawa Ghasia alipokuwa akitoa taarifa ya kamati yake amesema kuwa Kamati yake inardhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kusimamia Sheria ya Bajeti na kanuni zake ambayo inahakikisha usimamizi na uwajibikaji katika hatua zote za mchakato wa bajeti unazingatiwa.

Naye Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Halima Mdee alipokuwa akiwasilisha hotuba yake amesema kuwa Kambi Rasmi inaunga mkono hatua za kisheria zinazochukuliwa na Serikali kwa wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuhujumu uchumi wa nchi.

Post a Comment

0 Comments