Business

header ads

MBUNGE GODBLESS LEMA AFIKISHWA POLISI KWA MAHOJIANOMbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amesafirishwa kutokaMkoani Dodoma usiku wa kumkia jana na kuswekwa kwa mara nyingine tena Mahabusu Mkoani Arusha kwa mahojiano ya kosa la kutoa lugha za uchochezi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake , Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo, amesema Lema wamemweka mahabusu mpaka watakapomaliza mahojiano. 


Amesema kuwa endapo watamaliza mahojiano atafikishwa mahakamani wakati wowote, ili kujibu makosa anayokabiliwa nayo.

Kamanda Mkumbo amesema Lema amekuwa akitoa maneno na lugha za uchochezi na kuzirudia kila mara, hivyo wameona vema wamweke ndani.

Amesema jana walimkamata na kumuhoji, kisha kumwachia kwa dhamana, lakini kuna baadhi ya makosa hakuhojiwa, sasa ndio wanamuhoji.

Post a Comment

0 Comments