Business

header ads

MARUFUKU WAPIMAJI WA SERIKALI KUWA NA KAMPUNI BINAFSI ZA UPIMAJI

Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amesema kuwa serikali inapoteza mapato kutokana na kuwa na sehemu kubwa ya ardhi kutopimwa ambapo amewataka wataalam wafanye kazi ya kupima ardhi ili kuweza kuondokana na makazi holela.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo amesema mabadiliko ya kuondokana na mfumo wa hati kwenye karatasi na kuingia katika mfumo wa kieletroniki yatasaidia kuondoa tatizo la wananchi kudhulumiwa ardhi kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu.

Waziri Lukuvi amesema ni marufuku kwa wapimaji ardhi walioajiriwa na serikali kuwa kampuni za upimaji wa ardhi ili kuondokana na mgongano wa kimasilahi na kuwa katika miaka 10 ijayo kuwa kila mtu kuwa hati na kiwanja au shamba kiwe kimepimwa.

Nae Rais IST, Martins Chodata amesema kuwa watashirikiana na serikali katika masuala ya upimaji ardhi.Amesema wapo baadhi ya wapimaji ardhi hawana maadili na kusababisha kuwepo migogoro. 

Post a Comment

0 Comments