Business

header ads

MAJINA YA WASANII WANAOWANIA TUZO ZA EATV AWARDS KUANZA KUTANGAZWA


Kituo cha Habari cha East Africa Television (EATV) kuanzia kesho kitaanza kutangaza rasmi wasanii walioteuliwa kuwania tuzo za EATV AWARDS 2016 katika vipengelea mbalimbali ambavyo wasanii hao watachuana.

Zoezi la kutangaza wasanii hao walioteuliwa kuwania tuzo za EATV AWARDS, litafanyika katika maeneo tofauti ya Dar es Salaam kwa siku tofauti ambapo litaanza kesho Novemba 8, kuanzia saa 10 Jioni hadi Saa 11 jioni na kurushwa Live na EATV pamoja na East Africa Radio kutokea Mbagala Zhakiem.

Zoezi hilo la utangazaji wasanii watakaowania tuzo katika vipengele mbalimbali litaendelea Novemba 9 katika eneo la Karume kuanzia saa 10 hadi saa 11 jioni, Novemba 10 litaendelea tena kutangaza vipengele vingine katika eneo la Mabibo Hostel kuanzia saa 10 hadi saa 11 jioni na kisha kukamilishwa Novemba 11 huko Slipway kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa tano asubuhi.

Usikose kufuatilia mchakato mzima ili kupata kujua wasanii wako wakali watakaowania tuzo hizi kubwa kabisa Afrika Mashariki za EATV AWARDS, hapa East Africa Television na East Africa Radio.

Post a Comment

0 Comments